IQNA

Uislamu unaenea kwa kaasi

Wageni zaidi ya 347,000 wamesilimu Saudia ndani ya miaka mitano

18:51 - January 21, 2024
Habari ID: 3478226
IQNA - Kulingana na serikali ya Saudi Arabia, zaidi ya watu 347,000 wamesilimu nchini humo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Da'awa, na Miongozo ilitangaza kwamba imeajiri wahubiri 423 wa kigeni na jumuiya 457 za Da'awah katika maeneo mbalimbali ya ufalme huo ili kueneza Uislamu na kuwaalika wasio Waislamu kukumbatia imani hiyo, Gazeti la Saudi liliripoti Jumamosi.

Ripoti hiyo haikutoa maelezo yoyote kuhusu utaifa au asili za watu waliosilimu.

Hata hivyo, duru zinadokeza kuwa  waliosilimu ni wahamiaji wanaoishi na kufanya kazi nchini Saudi Arabia.

Ripoti hiyo pia inaonyesha mwelekeo wa ongezeko la wanaosilimu nchini humo. Mnamo 2019, kulikuwa na watu 21,654 waliosolimu Saudi Arabia wakati mnamo 2023, idadi hiyo ilifika163,319.

Kulingana na Kituo cha Utafiti cha Pew, Uislamu ndiyo dini inayokua kwa kasi zaidi duniani, ambayo inaweza kuelezewa na utandawazi, uhamiaji, miongoni mwa sababu nyinginezo.

Ni jambo la kuzingatiwa kuwa, idadi kubwa ya Wamagharibi wanaukumbatia Uislamu maishani pamoja na kuwepe propaganda dhidi ya Uislamu katika nchi zao.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Cambridge Press mnamo 2023 ulibaini kuwa kati ya Waislamu 1,034 wa Australia waliohojiwa, asilimia 15.8 walijitambulisha kama waliosilimu.

Vile vile, ripoti ya Pew Research mwaka 2017 ilionyesha kuwa asilimia 20 ya Waislamu 1,001 waliohojiwa nchini Marekani walikuwa waliosilimu, na wengi wao (asilimia 57) walikuwa Wakristo wa Kiprotestanti au Waorthodoksi.

3486883

Kishikizo: silimu saudia waislamu pew
captcha