IQNA

Nani Alikuwa Mjumbe wa Mwisho wa Mwenyezi Mungu

14:56 - September 13, 2023
Habari ID: 3477593
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu na historia, Muhammad (SAW) ndiye mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu.

 

Qu’rani Tukufu inasema;  Mtume Muhammad (SAW) si baba wa yeyote katika wanaume wenu, Yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Muhuri wa Mitume, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu, Tafsiri Aya ya 40 ya Surah Al-Ahzab.

Lakini kwa nini mkondo wa utume uliishia kwa Muhammad (SAW)

Wanabadilisha maji ya bwawa yanapochafuka na kuwa machafu, Wanatengeneza mtaa, nyumba, kipande cha nguo, gari n.k pindi vinapoharibika na kuhitaji kutengenezwa, Haja ya nabii mpya hutokea wakati kuna upotoshaji katika kitabu na mafundisho ya nabii aliyepita Wakati hakuna mabadiliko na upotoshaji hata kidogo katika Qur’ani Tukufu, hakuna haja ya mjumbe mpya waMwenyezi Mungu.

Licha ya vitabu vya Mwenyezi mungu vilivyotangulia kama vile Taurati na Biblia, ambamo ndani yake kuna upotoshaji, hakujakuwa na upotoshaji wowote katika Qur’ani Tukufu.

Pia tunapaswa kukumbuka kwamba sio wajumbe wote wa  Mwenyezi Mungu walikuwa na kitabu Kitukufu.

Idadi ya Manabii wa Mwenyezi mungu

Jambo lingine ni kwamba mtu asiyejua kusoma na kuandika anapotaka kwenda kwenye anwani mpya, angehitaji kuuliza njia katika kila uchochoro na barabara hadi atakapofika kule anakokwenda, Lakini mtu anayeweza kusoma atahitaji tu ramani ya jiji na mitaa yake ili kupata anwani.

Jamii inapofikia hatua fulani ya ukuaji, haihitaji tena kuongozwa moja kwa moja na manabi,. Bila shaka, mwongozo wa Maimamu maasum (AS) na Faqihi kwa ajili ya kutoa ushauri na kulinda mafundisho na sheria za kidini ni muhimu.

Mafaqihi waadilifu na wenye elimu ambao wamejizatiti na sheria za jumla za dini, wanaweza daima kutoa mafundisho na hukumu za Mwenyezi Mungu kutoka katika Qur’ani Tukufu na Hadithi.

 

3485110

Kishikizo: mtume muhammad
captcha