IQNA

Historia ya Uislamu

Maeneo matakatifu ya Iraq katika kumbukizi ya Kufariki Mtume Muhammad(SAW)

21:15 - September 14, 2023
Habari ID: 3477596
BAGHDAD (IQNA) – Mamia kwa maelfu ya wafanyaziyara wamesafiri katika miji mitukufu ya Iraq katika kumbukumbu ya kufariki Mtume Muhammad (SAW) na kuuawa shahidi mjukuu wake, Imam Hassan (AS).

Haram tukufu za Imam Ali (AS) huko Najaf na Imam Hussein (AS) na Hadhrat Abbas (AS) huko Karbala zimefunikwa na mabango meusi kwa mnasaba wa kumbukumbu ya matukio hayo ya huzuni.

Taratibu tofauti za maombolezo, hotuba za kidini na programu zingine hufanyika katika maeneo matakatifu siku hiI.

Wakati huo huo, Vikosi vya Ulinzi vya Kujitolea vya Wananchi (PMU), ambavyo pia vinajulikana kama Hashd al-Shaabi, vinatekeleza mpango mkubwa wa usalama ili kuhakikisha usalama wa wafanyaziyara wanaotembelea miji hiyo mitakatifu.

Siku ya 28 ya mwezi wa Safar (mwezi wa pili katika kalenda ya mwandamo wa Hijri) ni kumbukumbu ya kuaga dunia Mtume Muhammad (SAW) pamoja na kuuawa shahidi Imam Hassan (AS), Imam wa pili wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

3485174

captcha