IQNA

Umoja wa Kiislamu

Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu Kufanyika Tehran

18:48 - September 27, 2023
Habari ID: 3477659
TEHRAN (IQNA)- Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu wiki hii amezungumza na waandishi habari kuhusu Kongamano la 37 la Umoja wa Kiislamu mjini Tehran.

Hujjatul Islam  Hamid Shahriari alisema Jumatano kwamba wasomi 240 watatoa mihadhara katika mkutano huo, ambapo  kati yao wahadhiri 120 ni Wairani na 120 ni wa kigeni.

Mikutano kumi na sita ya mtandaoni itafanyika na ambapo  110 wasomi  Wairani Irani watawasilisha maoni yao. Shahriari kuongeza kuwa kutakuwa na mkutano mwingine wa mtandaoni ambapo utajumuisha wasomi Waislamu kutoka nchi mbali mbali duniani. Kongamano la ana kwa ana litaanza Jumapili na kumalizika Jumanne jijini Tehran

Mkuu wa Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu amesema katika kongamano hilo kutazinduliwa vitabu 15 na kuongeza kuwa wasomi wametuma makalaa 205 ambazo zitawasilishwa katika kongamano hilo. Akifafanua kuhusu baadhi ya malengo ya kongamano la mwaka huu la Umoja wa Kiislamu, Hujjatul Islam Shahriari amesema: INSERT SHAHRIARI.

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu inalenga kusambaza makongamano kama hayo katikak eneo. Tunataka kuonyesha kuwa, katika kipindi chote cha historia na hasa katika zama zenye kunawiri za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Waislamu wa madhehebu ya Shia na Sunni wamekuwa wakiishi pamojakwa maelewano. Hata katika Iran ya Kiislamu, Shia na Sunni wamekuwa wakishirikiana na kufanya kazi pamoja.

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu Iran hufanyika katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW, siku ambazo ni maarufu kama siku za Maulidi. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal. Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu.

4171474

captcha