IQNA

Kundi la kigaidi lahujumu hoteli Mali, 13 wauawa

15:25 - August 08, 2015
Habari ID: 3340139
Nchini Mali watu wasiopungua 13 wakiwemo wanajeshi watano wa serikali wameuawa Ijumaa na Jumamosi katika hujuma dhidi ya hoteli moja eneo la kati mwa nchi hiyo huku raia kadhaa wa kigeni wakichukuliwa mateka.

Imearifiwa kuwa watu waliokuwa na silaha wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi linalojiita Ansar Din walivamia Hoteli ya Byblos katika mji wa Sevare mapema Ijumaa kwa lengo la kuwachukua mateka raia wa nchi za Magharibi katika hoteli hiyo.
Hoteli hiyo pia inatumiwana wafanyakazi wa Kikosi cha Umoja wa Mataifa Mali MINUSMA. Katika taarifa, MINUSMA imesema wafanyakazi wake kadhaa wameuawa katika hujuma hiyo. Maafisa wa jeshi la Mali wameivamia hoteli hiyo na kuwanusuru raia kadhaa wa kigeni.
Kundi la Ansar Din linjidai kuwa la Kiislamu lakini linaeneza ugaidi na itikadi potofu na limetumia pengo la madaraka nchini  Mali kueneza satwa katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.../mh

3339982

Kishikizo: mali serikali kigaidi ansar
captcha