IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'an Tukufu nchini Mali waenziwa

18:55 - February 15, 2024
Habari ID: 3478357
IQNA - Sherehe za kufunga mashindano ya kitaifa ya Qur'ani katika nchini Mali ilifanyika mapema wiki hii.

Mashindano hayo yaliandaliwa mwezi Januari na Jumuiya ya Vituo vya Kuhifadhi Qur'ani nchini kwa msaada wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudia, tovuti ya al-Hadath iliripoti.

Washindani wapatao 100 walishindana katika sehemu mbili tofauti za wanaume na wanawake katika kategoria za kuhifadhi Qur'ani nzima pamoja na tafsiri ya aya, kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi nusu ya Qur'ani na kuhifadhi robo moja ya Qur'ani.

Mashindano hayo yaliandaliwa kwa lengo kuu la kutekeleza maamurisho ya Qur'ani Tukufu, kukuza kuhifadhi na kufasiri Qur'ani na kuwahimiza wahifadhi kuimarisha ujuzi wao wenye hadhi ya juu

Sherehe ya kufunga, ambapo washindi walitajwa na kutunukiwa, ilifanyika Jumatatu, Februari 12.

Mjumbe wa Saudia na baadhi ya viongozi wakuu wa kidini, kisiasa na kijamii wa Mali walihudhuria hafla hiyo.

Hafla ilianza kwa qiraa ya aya za Qur'ani Tukufu ikifuatiwa na hotuba ya waziri wa masuala ya kidini wa Mali, Mohammed Omar.

Aliwashukuru waandaaji wa mashindano hayo na kusema programu hizo zinakuza shughuli za Qur'ani na kutumikia Kitabu Kitukufu.

Washindani wakuu katika sehemu za wanaume na wanawake walitunukiwa zawadi na vyeti vya heshima.

Jamhuri ya Mali ni nchi isiyo na bahari Afrika Magharibi katika ukanda wa Sahel na ni nchi ya nane kwa ukubwa barani Afrika. Idadi kubwa ya wakazi wa Mali ni Waislamu.

 

4199674

captcha