IQNA

ISESCO yalaani hujuma za kigaidi Ankara, Uturuki

11:27 - October 11, 2015
Habari ID: 3384025
Jumuiya ya Kiutamaduni, Kisayansi na Kielimu ya Nchi za Kiislamu ISESCO imetoa taarifa na kulaani vikali mlipuko wa jana katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara.

Jumuiya ya Kiutamaduni, Kisayansi na Kielimu ya Nchi za Kiislamu ISESCO imetoa taarifa na kulaani vikali mlipuko wa jana katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara.
Katika taarifa, ISESCO imesema magaidi waliotekeleza ukatili huo hawana hawaheshimu damu ya raia wasio na hatia. ISESCO imesema magaidi ni vibaraka ambao wanalenga kuibua ufisadi na kueneza vita vya kimadhehebu katika eneo.
ISESCO na imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuunga mkono vita dhidi ya ugaidi.
Jana asubuhi wasiopungua 97 wameuawa katika milipuko miwili iliyotokea mapema leo katikati ya mji mkuu wa Uturuki, Ankara. Watu wengine karibu 200 kujeruhiwa huku 28  kati yao wako katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Rais wa Uturuku, Recep Tayyep Erdogan amelaani vikali hujuma hiyo na kusema imelenga umoja na amani ya nchi hiyo. Amesisitiza kuwa azma na mshikamano utakaoonyeshwa na wananchi baada ya hujuma hiyo litakuwa jibu kali zaidi kwa ugaidi huo.../

3383919

captcha