IQNA

Turathi za Kiislamu

Msikiti wa Kale wa Irani Umeteuliwa kwa Lebo ya ICESCO

22:57 - August 05, 2023
Habari ID: 3477385
TEHRAN (IQNA) - Iran imeteua msikiti wake wa Tarikhaneh, ambao ulijengwa takriban miaka 900, kwa ajili ya kuwekwa katika orodha turathi ya Jumuiya ya Kiislamu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (ICESCO).

ISESCO ambayo inalenga  kusaidia kuhifadhi na kukuza maeneo mashuhuri ya urithi wa kitamaduni, inatarajiwa kutangaza orodha ya washindi mwishoni mwa msimu wa joto mwaka huu..

Ripoti hiyo ilisema kuwa msikiti huo wa matofali ya udongo, ulioko karibu na mji wa kisasa wa Damghan katika mkoa wa Semnan, unatarajiwa kupata nafasi kwenye Orodha ya Turathi ya Dunia wa Kiislamu ya ICESCO (IWHL).

Msikiti huo ambayo pia huitwa Tarik Khana, pia ni maarufu likana kama msikiti "mkongwe zaidi unaotumika" nchini Iran.

Kwa mtazamo wa usanifu, msikiti huu wa matofali ya matope unajumuisha muundo sahali wa Waarabu na mbinu za ujenzi za zama za  watawalawa Sassani nchini Iran.

Mji wa kale wa Damghan ulikuwa mji mkuu wa majira ya baridi wa wafalme wa Parthian. Ukiwa na takriban kilomita 350 kaskazini-mashariki mwa Tehran, Damghan wakati mmoja ulikuwa mji wenye mafanikio kwenye Barabara ya Hariri iliyounganisha China na Asia Magharibi na Ulaya. Masimulizi yanasema kwamba Damghan iliwahi kuitwa jiji lenye  milango mia moja. Baadaye, wakati wa utawala wa Sassani, Umayya, Abbasi, Taheri, Samani, Sarbedaran, na nasaba za Deylamite, mji wa Damghan ulikuwa na nafasi kubwa kwa magavana.

Likiwa na makao yake makuu mjini Rabat, Morocco, Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (ICESCO, zamani ISESCO) lilianzishwa na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu mnamo Mei 1979. Lina nchi wanachama 54.

Ni shirika maalumu linalojihusisha na nyanja za elimu, sayansi, utamaduni, na mawasiliano katika nchi za Kiislamu ili kusaidia na kuimarisha uhusiano kati ya nchi wanachama.

3484645

Kishikizo: isesco iran
captcha