IQNA

Misikiti 10 kujengwa nchini Mali

13:12 - November 19, 2015
Habari ID: 3454532
Misikiti 10 mipya inatazamiwa kujengwa nchini Mali magharibi mwa Afrika kupitia ufadhili wa Taasisi ya Misaada ya RAF.

Kwa mujibu wa tovuti ya al Arab, misikiti hii itajengwa katika fremu ya mpango maalumu wa kujenga misikiti na vituo vha Kiislamu katika nchi mbali mbali duniani. Mpango huo unadhaminiwa na Taasisi ya Qatar ya Misaada ya Kibinadamu ya Sheikh Thani bin Abadalla kwa kifupi RAF.
Misikiti hiyo inatazmaiwa kujengwa katika vijiji vya watu wasiojiweza kifedha. Mbali na jengo kuu la ibada, misikiti hiyo pia itakuwa na maktaba ya umma.
Uislamu uliingia Mali miaka elfu moja iliyopita na nchi hiyo ni kati ya nchi zenye turathi za kale zaidi za Kiislamu barani Afrika. Mji wa Timbuktu nchini Mali ni moja kati ya vituo muhimu vya turathi za utamaduni wa Kiislamu Afrika na duniani kote. Waislamu ni zaidi ya asilimia 90 ya watu wote milioni 15 nchini Mali.../

3454520

captcha