IQNA

Mashhad, Mju Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu 2017+PICHA

16:37 - January 04, 2017
Habari ID: 3470781
IQNA-Mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran umezinduliwa rasmi kama Mji Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2017.

Hafla za uzinduzi huo zilifanyika Jumatatu na kuhudhuria na Waziri wa Utamduni na Muongozo wa Kiislamu Iran Seyed Reza Salehi Ammiri pamoja na mkuu wa mkoa wa Khorassan Razavi Ali Rashidian.

Katika uzinduzi huo nembe ya " Mashhad, Mju Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu 2017" pia ilizinduliwa.

Halikadhakila waziri wa utamaduni walifanya ziara katika Haram Takatifu ya Imam Ridha AS katika mji huo wa Mashhad.

Katika kongamano la 7 ya Shirika la Kiislamu la Elimu,Sayansi na Utamaduni ISESCO liliteua mji wa Mashhad kuwa mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2017.

Kila mwaka Mashhad huwa mwenyeji wa wafanyaziara milioni 27 Wairani na milioni mbili kutoka nje ya Iran ambao hufika hapo kufanya ziara katika Haram Takatifu ya mjukuu wa Mtume Muhammad SAW, Imam Ridha AS.

ISESCO ilianzishwa na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC mnamo mwezi Mei 1979.

ISESCO ina nchi wanachama 52 ina ni kati ya jumuiya kubwa zaidi za Kiislamu katika sekta ya elimu sayansi na utamaduni ambapo makao yake makuu yako Rabat, Morocco.

Mashhad, Mju Mkuu wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu 2017

3461848/

captcha