IQNA

Katika Mkutano wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Morocco

Nchi za Kiislamu zatakiwa kusaidia vyuo vikuu Palestina

9:35 - February 16, 2017
Habari ID: 3470852
IQNA:Mkutano wa saba mkuu wa Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu katika kulinda utambulisho wa Kiislamu wa "Quds Tukufu" umefanyika nchini Morocco.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA , wakuu wa vyuo vikuu vya ulimwengu wa Kiislamu wameshiriki kwenye mkutano huo na kuunga mkono hatua za Chuo Kikuu cha Quds huko Palestina cha kushikamana na muqawama na kusimama kidete kukabiliana na jinai za utawala ghasibu wa Israel na kulinda utambulisho wa Kipalestina na Kiislamu wa mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas.

Washiriki wa mkutano huo wamehimiza mshikamano na kuwa kitu kimoja vyuo vikuu vya umoja huo na kukiunga mkono na kukisaidia kwa kila namna Chuo Kikuu cha Quds.

Mkutano huo umezitaka pia taasisi za Kiarabu, Kiislamu na za kimataifa zinazohusiana na masuala ya elimu ya juu kuzisaidia taasisi za vyuo vikuu vya mji wa Baytul Muqaddas na Palestina kiujumla, hususan Chuo Kikuu cha Quds.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu umefanyika tarehe 13 na 14 mwezi huu wa Februari nchini Morocco, kwa kuwashirikisha wakuu vya vyuo vikuu mbalimbali vya ulimwengu wa Kiislamu akiwemo Muhammad Kafi, mkuu wa Chuo Kikuu cha Firdousi cha mjini Mash'had Iran.Nchi za Kiislamu zatakiwa kusaidia vyuo vikuu Palestina

Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu uliasisiwa mwaka 1987 chini ya Taasisi ya Kiislamu ya ISESCO na hivi sasa vyuo vikuu na taasisi 314 za elimu ya juu ni wanachama wa umoja huo.

3574713

captcha