Taarifa iliyotolewa na Hizbullah imesema kuwa, mapema leo, kambi za jeshi la utawala wa Kizayuni Israel katika eneo la Lebanon linalokaliwa kwa mabavu na utawala huo la Mashamba ya Shebaa zimeshambuliwa kwa makumi ya maroketi ya wapiganaji wa harakati hiyo.
Taatifa hiyo ya Hizbullah imeongeza kuwa, mashambulizi hayo ni jibu kwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa jana na utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo kadhaa ya miiniko ya Kafr Shuba.
Kufuatia mashambulizi hayo ya kulipiza kisasi, Waziri Mkuu wa Israeli Naftali Bennett na Waziri wa Vita, Benny Gantz walifanya kikao cha dharura kujadili suala hilo
Televisheni ya Al Mayadeen ya Lebanon imesema maroketi yasiyopungua 20 yalirushwa dhidi ya vituo vya jeshi la Israeli. Televisheni ya Al-Minar pia imesema maroketi kadhaa yalilenga kituo cha jeshi la Israel cha Douf.
Aoun pia amesema mashambulizi hayo ya Israel ni tishio la moja kwa moja kwa usalama na amani ya kusini mwa Lebanon na yamekiuka maazimio ya Baraza la Usalama la UN.