IQNA

Mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Mali wafanya mazungumzo mjini Tehran

22:01 - February 13, 2022
Habari ID: 3474927
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran leo Jumapili na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali aliyeko ziarani hapa nchini.

Abdoulaye Diop Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali ambaye yuko ziarani hapa nchini kwa minajili ya kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Iran leo amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  

Abdoulaye Diop Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali kabla ya kufanya mazungumzo na Amir Abdollahian alikuwa ameonana na Muhammad Ali Zolfi Gol Waziri wa Sayansi, Utafiti na Teknolojia wa Iran ambapo alisema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kigezo kizuri kwa nchi nyingine zinazotaka kuendesha mapambano dhidi ya  uistikbari na vikwazo vya kidhalimu kutokana na nafasi ya juu iliyonayo kwa upande wa sayansi na teknolojia duniani.  

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine licha ya kukabiliwa na vikwazo na kupambana na adui lakini imefikia katika nafasi ya juu. Amesema Mali ina hamu ya kustafidi na uzoefu wa Iran kwa ajili ya ustawi wa sayansi na teknolojia wa nchi hiyo. 

/670080

captcha