IQNA

Harakati ya kuwatetea mateka wa Kipalestina katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel

19:21 - February 28, 2022
Habari ID: 3474986
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya mateka wa Kipalestina katika magereza ya utawala dhalimu wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuanza harakati ya Intifadha au mwamako wa wafungwa wa Kipalestina na kutoa wito wa kuungwa mkono harakati hiyo.

Kamati ya Dharura yenye mfungamano na harakati ya mateka wa Kipalestina katika magereza ya utawala ghasibu wa Israel imetangaza kuwa, Intafadha ya wafungwa wa Kipalestina katika magereza ya Israel haitosita mpaka pale matakwa ya mateka na wafungwa wa Kipalestina yatakapotekelezwa kikamilifu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kwa kuzingatia hatua zisizo za kibinadamu zinazotekelezwa na utawala vamizi wa Israel, kumeibuka mgomo mkubwa wa kususia chakula ukiwashirikisha wafungwa wote.

Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, utawala wa Kizayuni wa Israel umesambaza kwa makusudi virusi vya corona katika jela ya mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa na utawala huo.

Hii ni katika hali ambayo, katika siku za hivi karibuni kitongoji cha Sheikh Jarrah katika eneo la Quds kimekumbwa na mashambulizi makubwa yanayofanywa walowezi na wanajeshi wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina.

Makumi ya familia za Kipalestina zinazoishi katika kitongoji hicho ziko hatarini kuhamishwa kwa nguvu na utawala vamizi wa Kizayuni wa Israel.

Vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina ni mfano wa wazi wa ubaguzi wa apartheid kwa mujibu wa kifungu cha 2 cha Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Uhalifu wa Ubaguzi.

4039307

Kishikizo: palestina mateka israel
captcha