IQNA

Wafungwa Wapalestina wamshukuru Sayyid Nasrallah wakiwa mahakamani Israel + Video

21:30 - December 08, 2021
Habari ID: 3474657
TEHRAN (IQNA)- Wafungwa Wapalestina wakiwa katika mahakama moja ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Nazareth wamempongeza Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah Sayyed Hassan Nasrallah.

Wafungwa hao watatu ambao waliwahi kutoroka jela na kisha kukamatwa,  Iyad Jradat, Ali Abu Bakr na Mahmoud Shreim, walifikishwa katika mahakama ya Israel.

"Tunamshukuru Sheikh (Sayyid) Hassan Nasrallah, ambaye alikuwa amewataka ndugu zetu katika Hizbullah wawe tayari mpakani kuwapokea (Wapalestina) waliotoroka jela," Jradat ameiambia mahakama.

Alikuwa akiashiria tukio la  mwezi Septemba mwaka huu ambapo mateka 6 wa Kipalestina wametoa pigo kali kwa hadhi ya utawala wa Kizayuni wa Israel kwa hatua yao ya kuchimba njia ya chini ya ardhi iliyopewa jina la "Handaki ya Uhuru". Mateka hao sita walichimba njia ya chini ya ardhi na kufanikiwa kutoroka jela ya Gilboa yenye ulinzi mkali ya utawala haramu wa Israel. 

Mateka wanne Wapalestina walikamatwa Septemba 11 baada ya siku sita za uhuru wakiwa wakiwa bado ndani ya Israel (ardhi zinazokaliwa kwa mabavu) na wengine wawili walikamatwa Septemba 19 katika mji wa Jenin wa Ukingo wa Magharibi.

Katika hotuba ya Septemba 13 Sayyid Hassan Nasrallah alisema wapiganaji wa Hizbullah walikuwa tayari katika mpaka wa Lebanon kuwapokea Wapalestina walikuwa wanatoroka jela za Israel.

Wakati Wapalestina hao walipotoroka gereza, Hizbullah ilisema kitendo hicho ni pigo kubwa kwa utawala wa Kizayuni ambapo unakalia ardhi za Palestina kwa mabavu. Hizbullah imesema kitendo hicho cha kutoroka jela yenye ulinzi mkali ni cha kipekee na kuongeza kuwa, “kitendo hicho ni ushahidi wa wazi wa ustadi, subira na mapambano yanayoendelea ya Wapalestina kwa lengo la kukomboa ardhi zao na wafungwa.”

3476847

captcha