IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Balozi wa Saudi Arabia apongeza Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

21:12 - February 18, 2024
Habari ID: 3478374
IQNA - Balozi wa Saudi Arabia nchini Iran amepongeza mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni muhimu sana na yenye thamani kubwa.

Balozi Abdullah bin Saud al-Anzi alitembelea ukumbi wa Awamu ya 40 ya  Kimataifa ya Qur'ani ya Iran jijini Tehran Jumamosi jioni.

Alimtazama mhiriki Saudia akiwa jujuani na vile vile washiriki kutoka Lebanon, Palestina na washiriki wengine kadhaa.

Kama ilivyoamrishwa na jopo la majaji, qari wa Saudia alisoma Aya ya 21 na 22 za Surah An-Nur:

Alipoulizwa na mwandishi wa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) kuhusu tathmini yake ya tukio hilo Qur'ani, balozi wa Saudia aliyataja mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran kuwa "muhimu na yenye thamani kubwa."

Al-Anzi ameongeza kuwa, ushiriki wa mwakilishi wa Saudi Arabia unaenda sambamba na kuthamini umuhimu wa mashindano hayo.

Saudi Envoy Lauds Iran’s Int’l Quran Contest

Alipoondoka kwenye ukumbi wa mashindano, al-Anzi alizungumza na qari wa Saudia, akapongeza utendaji wake na kumtakia mafanikio.

Fainali ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ilianza Alkhamisi mjini Tehran kwa kauli mbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja, Kitabu cha Muqawama au Mapambano".

Kwa mujibu wa waandaaji, zaidi ya nchi 110 zilijiandikisha kushiriki mashindano hayo na walioingia fainali  ni washiriki 69 kutoka nchi 44.

Mashindano hayo yataendelea hadi Jumanne, Februari 20, na washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga Jumatano, Februari 21.

3487229

Habari zinazohusiana
captcha