IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani

Iran imeandaa vikao 270 vya Kusoma Qur'ani wakati wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani

20:16 - February 20, 2024
Habari ID: 3478381
IQNA - Sambamba na Awamu ya 40 ya Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran, ambayo yamekuwa yakiendelea mjini Tehran tangu Alhamisi, nchi kote Iran kumeandaliwa vikao 270 vya usomaji Qur'ani katika miji tofauti.

Seyed Mohammad Mojani, mkuu wa kamati ya kiufundi ya mashindano hayo, alisema programu za Qur'ani zimepangwa kando ya mashindano hayo kwa maelekezo ya mkuu wa Shirika la Iran la Wakfu na Missad.
Idara za Wakfu mjini Tehran na majimbo mengine zimekuwa zikifanya programu hizo kuanzia Februari 15 na zitaendelea hadi Februari 21, alisema.
Wasomaji au maqari mashuhuri husoma Qur'ani Tukufu katika vikao vya Qur'ani, afisa huyo alibainisha.
Ripoti ikijumuisha maelezo zaidi kuhusu programu hizo itawasilishwa wakati wa mkutano wa washiriki wa mashindano hayo na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu baadaye wiki hii, aliendelea kusema.

Fainali ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Iran  ilizinduliwa mjini Tehran siku ya Alhamisi na itaendelea hadi Februari 21.

Jumla ya wahifadhi na wasomaji 69 kutoka nchi 44 wanashindana katika fainali katika kategoria kuu za usomaji wa Qur'ani (kwa wanaume) na kuhifadhi Qur'ani na usomaji wa Tarteel (kwa wanaume na wanawake).

Hafla hiyo ya kila mwaka, inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

3487267

Habari zinazohusiana
captcha