IQNA

Siku ya Tatu ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran-VIDEO

14:33 - February 19, 2024
Habari ID: 3478379
IQNA - Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaJamhuri ya Kiislamu ya Iran yaliendelea Jumapili, Februari 18, huku washiriki wa mataifa mbalimbali wakipanda jukwaani.

Siku ya Jumapili na katika kitengo cha wanaume, wasomaji na wahifadhi sita walipanda jukwaani kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Tehran, wakionyesha ujuzi wao wa kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu.

Obaidullah Boubkrango kutoka Niger alikuwa mshiriki wa kwanza ambaye alitoa majibu kwa maswali ya jopo la majaji katika kitengo kizima cha kuhifadhi Qur'ani.

Mehdi Chamouni from Lebanon was the next qari who recited verses 160-166 of Surah Al-Imran.

Abdul Manan Ahmed Fauzi wa Indonesia alikuwa mshiriki aliyefuata ambaye alisoma aya za 53-64 za Surah Al-Ma’idah katika kitengo cha kisomo cha Tarteel.

Mshiriki aliyefuata alikuwa Deramy Ismail kutoka Ivory Coast ambaye alijibu maswali kutoka kwa majaji katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani.

Mustafa Brannon kutoka Thailand alisoma aya za 19-25 za Surah Al-Ankabut katika kategoria ya qiraa.

Bilal Sheikh Khaled wa Syria alikuwa mshiriki wa mwisho ambaye alisoma kwa Tarteel  aya za 104-113 za Surah At-Tawbah.

i. Mashindano hayo yaliyoanza siku ya Alkhamisi yamewavutia wapenzi wa Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwemo viongozi na watu mashuhuri wa Iran. Zaidi ya nchi 110 zilijiandikisha kwa shindano hilo, lakini ni wahitimu 69 tu kutoka nchi 40 waliofanikiwa kuingia katika duru ya mwisho baada ya mchakato mkali wa mchujo.
Mashindano hayo yataendelea hadi Jumanne, Februari 20, na washindi watatunukiwa katika hafla ya kufunga Jumatano, Februari 21. Hafla hiyo ya kila mwaka, inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

3487248

 

Habari zinazohusiana
captcha