IQNA

Rais Rouhani

Iran itaibuka mshindi katika kadhia ya nyuklia

15:09 - May 26, 2014
Habari ID: 1411319
Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itapata ushindi katika kuyakabili na hatimaye kuyaondoa mashinikizo dhidi ya miradi yake ya nishati ya nyuklia.

Akizungumza Jumapili mjini Tehran katika uufnguzu wa mkutano wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Radio na Televisheni za Kiislamu, Rais Rouhani alisema: “Katika suala la teknolojia ya nyuklia, sina shaka yoyote kuwa taifa la Iran litapata ushindi dhidi ya mashinikizo yanayotolewa na wengine” amesema Rais wa Iran. Ameongeza kuwa Iran itasonga mbele hatua kwa hatua huku ikidhamini haki zake kwa kutumia hoja na mantiki katika mazungumzo na kundi la 5+1. Dakta Hassan Rouhani amesisitiza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaendelea na mazungumzo na nchi hizo sita kuhusiana na shughuli zake za nyuklia hadi kuhakikisha vikwazo dhidi yake vinaondolewa moja kwa moja na kuiwezesha kumiliki kwa sura ya kudumu teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani. Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza pia kwamba Iran haitochukua hatua za utekelezaji nje ya mipaka aliyoielezea kuwa ya “kawaida, ya kisheria na ya uwazi” kuhusiana na haki zake za nyuklia na wala haitoruhusu maadui wakiuke haki zake hizo. Iran na nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, yaani Marekani, Russia, China, Uingereza na Ufaransa pamoja na Ujerumani zinaendelea na mazungumzo, zikiwa katika hatua ya kutatua hitilafu zilizopo baina ya pande mbili na kuanza kuandaa rasimu ya makubaliano rasmi yatakayohitimisha mzozo ulioanzishwa na madola ya Magharibi kuhusiana na miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani…/

1410564

Kishikizo: rouhani iran
captcha