IQNA

Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu

Mkutano wa Soko la Mitaji ya Kiislamu wafanyika Tehran

19:12 - November 26, 2023
Habari ID: 3477953
TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa 15 wa Kimataifa wa Soko la Mitaji ya Kiislamu (ICM) unafanyika, Tehran, mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo unashirikisha wataalamu na wasimamizi wa ndani na nje ya nchi.

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana  ya Iran (SEO) na Jumuiya ya Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu  Iran, linalenga kutangaza suhula za kifedha za Kiislamu na kushughulikia changamoto na fursa zao.

Mkutano huo wa siku mbili ulizinduliwa Jumapili na Majid Eshghi, mkuu wa SEO, ambaye aliwakaribisha waliohudhuria na kusisitiza umuhimu wa soko la mitaji la Kiislamu kwa maendeleo ya uchumi na jamii.

Mkutano huo unahusu mada mbalimbali zinazohusiana na soko la mitaji ya Kiislamu, kama vile utawala wa Shariah, dhamana za kifedha za Kiislamu, uwajibikaji kwa jamii, mfumo wa kifedha wa crypto, uwazi , suhula muda mfupi za ufadhili, suhula za ufadhili wa pamoja na mahitaji ya kisheria na udhibiti.

Kwa mujibu wa waandaji mkutano huo umevutia washiriki 42 kutoka Russia, Kuwait, Indonesia, Syria, Iraq, Pakistan, Maldives, Malaysia, Uturuki, India, pamoja na zaidi ya washiriki 200 wa Iran. Mkutano huo unatarajiwa kutoa jukwaa la kubadilishana mawazo na uzoefu, pamoja na kuimarisha ujuzi na utaalamu wa washiriki.

Islamic Capital Market Conference Opens in Tehran

3486177

captcha