IQNA

Haki za Wanawake katika Uislamu

Raisi: Magharibi inakiuka haki za wanawake, inawatumia kama chombo cha mashinikizo

18:52 - October 02, 2023
Habari ID: 3477684
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran anasema tofauti na Iran, nchi za Magharibi zimekuwa zikikiuka haki za binadamu kwa kuwatumia wanawake kama chombo cha mashinikizo dhidi ya mataifa huru.

Rais Ebrahim Raisi ameyasema hayo leo mjinii Tehran mbele ya hadhara ya washiriki katika "Tamasha la Kwanza la Kimataifa la Vyombo vya Habari la Khorsheed" na kuongeza kwamba: Wamagharibi wanatoa madai ya kutetea haki za wanawake ili kuwatumia kama wenzo tu. 

Sayyid Ebrahim Raisi amesema, Jamhuri ya Kiislamu inaamini kuwa nchi za Magharibi zinawatumia wanawake kama wenzo. Amesema, wanawake katika Mapinduzi ya Kiislamu  walikuwa na nafasi kubwa katika mapambano dhidi ya utawala dhalimu, na walikuwa na mchango mkubwa wakati wa kipindi cha kujihami kutakatifu, katika ujenzi mpya wa nchi na kwenye nyanja mbalimbali za kisayansi, kiutamaduni, kijamii, kisiasa na kimichezo.  

Rais Raisi ameongeza kuwa: Wamagharibi leo hii wanatumia suala la haki za wanawake kama wenzo wa kuzishinikiza nchi huru duniani na sio watetezi wa haki wa wanawake au haki za binadamu. Hii ni kwa sababu hiii leo tunashuhudia orodha ndefu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na wanawake katika jamii za Magharibi. 

Raisi ameendelea kubainisha kuwa: Ni miaka 70 sasa ambapo nchi za Magharibi zinapuuza haki za wananchi wa Palestina, na uvamizi wa nchi hizo huko Afghanistan umesababisha mauaji na uharibifu nchini humo.  

Amesema kuwa nchi za Magharibi, hasa Marekani, zinaendeleza ujinga mamboleo miongoni mwa mataifa kwa kutumia vyombo vya habari kupotosha ukweli, na kuficha habari za kweli.

Vilevile amezungumzia jinsi Wamagharibi wanavyokivunjia heshima kitabu kitakatifu zaidi cha Mwenyezi Mungu kwa kisingizio cha uhuru wa kusema, licha ya kwamba vitendo hivyo ni kinyume na uhuru wa kusema, dhidi ya fikra na dhidi ya ubinadamu.

 

4172632

Kishikizo: wanawake waislamu iran
captcha