IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Wasomaji Qur'ani mashuhuri duniani wajibu vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu (+Video)

15:08 - August 24, 2023
Habari ID: 3477485
TEHRAN (IQNA) – Idadi ya wasomaji Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu katika jumbe tofauti za video wamelaani vitendo vya kuvunjia heshima Qur’ani Tukkufu barani Ulaya, wakisisitiza kwamba hatua hizo zitashindwa kudhoofisha hadhi tukufu ya Kitabu hicho Kitukufu.

Muslim World’s Prominent Qaris React to Quran Desecrations in West

Katika wiki za hivi karibuni, shakhsia na makundi yenye chuki dhidi ya Uislamu katika nchi kadhaa za Ulaya mara kadhaa yametekeleza uchomaji moto wa Misahafu au nakala za Qur'ani Tukufu na majaribio kama hayo ya kukivunjia heshima Kitabu Kitukufu cha Waislamu.

Vitendo hivyo vya kufuru katika nchi za Uswidi, Denmark na Uholanzi vimeibua hasira na lawama kutoka kwa nchi za Kiislamu na dunia nzima.

Zifuatazo ni kauli za baadhi ya wasomaji Qur'ani mashuhuri wa ulimwengu wa Kiislamu kuhusu vitendo hivyo viovu.

4164243

Habari zinazohusiana
captcha