IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu: Polisi wa Uswidi wamlinda mchochezi Mpinga Uislamu

20:58 - September 04, 2023
Habari ID: 3477544
STOCKHOLM (IQNA) - Polisi wa Uswidi wamewakamata watu 15 ambao walijaribu kumzuia mtu mwenye msimamo mkali asichome Qur'ani Tukufu huko Malmo.

Polisi waliwakamata watu 15 huko Malmo, Uswidi, siku ya Jumapili baada ya makabiliano kati ya waandamanaji watetezi wa Qur'ani Tukufu na watu wenye itikadi kali dhidi ya Uislamu.

Salwan Momika, mkimbizi wa Iraq mwenye chuki dhidi ya Uislamu, alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu chini ya ulinzi wa polisi huko Varnhemstorget, kitongoji chenye idadi kubwa ya Waislamu.

Takriban waandamanaji 200 walijibu kwa kumrushia mawe na chupa Momika na polisi, wakijaribu kumzuia asichome Qur'ani Tukufu.

Maandamano hayo yalimalizika mapema kuliko ilivyopangwa huku polisi wakimzuilia Momika na kumkimbiza nje ya eneo hilo kwa gari.

Mwanaume mwingine alijitupa mbele ya gari, akijaribu kulizuia kuondoka. Polisi pia walimenyana na muandamanaji mwingine kabla ya kumkamata.

Tukio hili ni la hivi punde tu katika mtindo wa kutatanisha wa kudhalilishwa kwa Qur'ani Tukufu, hasa nchini Uswidi na Denmark.

Vitendo hivi vya kulaumiwa sio tu vimevuruga uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uswidi na mataifa ya Mashariki ya Kati bali pia vimesababisha mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Uswidi mjini Baghdad.

Wakati serikali ya Uswidi ilitoa shutuma za kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu siku za nyuma, wao wamesisitiza kutokuwa na uwezo wa kuzuia matukio hayo kutokana na sheria za uhuru wa kuzungumza. Kwa hivyo, matukio haya yameilazimisha Uswidi kuongeza kiwango cha vitisho vya ugaidi na kuimarisha hatua za usalama za mpaka.

Wakati huohuo, Denmark ambayo pia imeshuhudia kudhalilishwa hadharani kwa Qur'ani Tukufu, sasa inatafakari kupiga marufuku kuchomwa moto kitabu hicho kitakatifu cha Waislamu. Uswidi, pia, inachunguza njia za kisheria kushughulikia wasiwasi huu unaokua.

3485030

Habari zinazohusiana
captcha