IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Mkuu waJumuiya ya Waislamu Duniani ahimiza mazungumzo kkabiliana na kuvunjiwa heshima Qur'ani

17:45 - August 16, 2023
Habari ID: 3477447
STOCKHOLM (IQNA) - Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Duniani (MWL) amesema mgogoro wa kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu unapaswa kugeuzwa kuwa fursa ya mazungumzo.

Katika makala ya gazeti la kila siku la Uswidi la Dagens Nyheter, Muhammad bin Abdul Karim Issa alitoa wito kwa Uswidi na Waislamu kote ulimwenguni kuzuia njia kwa wale wanaotaka kueneza chuki.
Alisema kwa kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu, watu hao wanataka kuzusha mifarakano baina ya Waislamu na wasio Waislamu nchini Uswidi
Wanataka kuzuia mazungumzo kati ya Uswidi na ulimwengu wa Kiislamu na kueneza mizozo na tofauti, alisema.
"Wanataka kutugombanisha sisi wenyewe kwa wenyewe lakini imani yetu ya Kiislamu hairuhusu jambo kama hilo kutokea."
Issa aliongeza kuwa kuna fursa leo kwa ajili ya kufanya kile ambacho watu wanaochochea chuki wamekuwa wakijaribu kuzuia kwa muda mrefu, ambayo ni kuongeza ufahamu kwa watu wa Uswidi kuhusu Uislamu na maadili yake.
Wale wanaoichoma Qur'ani Tukufu bila kukusudia husababisha watu wengi Uswidi kuvutiwa zaidi na  Kitabu Hicho Kitukufu, aliendelea kusema.
Katika wiki za hivi karibuni, kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na Denmark kwa idhini ya serikali na ulinzi wa polisi kumezua hasira na shutuma nyingi kutoka kwa ulimwengu wa Kiislamu.
Nchi za Nordic zinaruhusu vitendo hivyo kutokea chini ya kivuli cha kile kinachoitwa uhuru wa kujieleza licha ya kulaumiwa vikali na mataifa ya Kiislamu na yasiyo ya Kiislamu na  Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa. 
4162805

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watetezi wa qurani
captcha