IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

TikTok yamzuia kupata pato aliyevunjia heshima Qur'ani Tukufu nchini Uswidi

13:26 - August 31, 2023
Habari ID: 3477524
STOCKHOLM (IQNA) - Mtu aliyechoma nakala za Qur'ani Tukufu nchini Uswidi sasa amezuiwa na mtandao wa kijamii wa TikTok kufaidika na klipu anazosambaza.

Maafisa wa TikTok walithibitisha kuwa jukwaa hilo la video fupifupi limezima kipengele kinachowawezesha watumiaji kutoa pesa kwa Salwan Momika, Redio ya Uswidi iliripoti.

Kuanzia sasa na kuendelea, watumiaji hawataweza kutumia kipengele cha "zawadi" cha TikTok wanapotangamana na video zilizosambazwa na Momika, ambaye amekivunjia heshima Kitabu Kitakatifu cha Waislamu katika mfululizo wa maandamano ya kupinga Uislamu ambayo yamezua hasira katika nchi nyingi za Kiislamu.

Hayo yanajiri wakato ambao gazeti la Aftonbladet limeripoti kwamba Momika alihukumiwa mwaka wa 2021 kwa kumtishia mtafuta hifadhi kutoka Eritrea kwa kisu alipokuwa akiishi katika makao ya wakimbizi.

Iliongeza kuwa Momika alihukumiwa saa 80 za kazi bila malipo hadharani na kuamriwa kulipa dola 1,000 za fidia kwa mtafuta hifadhi.

Mnamo Januari 21, Momika alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya Ubalozi wa Uturuki nchini Uswidi na Januari 27 nje ya Ubalozi wa Uturuki nchini Denmark.

Momika alichoma nakala ya kitabu kitakatifu cha Waislamu nje ya msikiti mmoja huko Stockholm mnamo Januari 28 wakati wa Eid al-Adha. Vitendo hivyo vinaendelea kulaaniwa vikali na Waislamu kote duniani.

3484990

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watetezi wa qurani
captcha