IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Polisi wa Uswidi wamzuia mtu aliyekuwa anapinga Uchomaji wa Qur'ani Tukufu

16:26 - August 25, 2023
Habari ID: 3477496
STOCKHOLM (IQNA) - Mwanamume mmoja ambaye alikuwa akiandamana kupinga mtu mwenye misimamo mikali aliyekuwa akichoma moto Qur'ani Tukufu mbele ya Msikiti wa Stockholm alizuiwa na polisi waliovalia kiraia.

Kais Tunisia, Mwislamu, alikuwa akionyesha hasira yake dhidi ya mtu mwenye msimamo mkali aliyekuwa akivunjia heshima Qur'ani Tukufu lakini afisa wa polisi alimzuia kubainisha hasira zake.

Tunisia ilisema anatumia uhuru wake wa kujieleza, lakini polisi walimuonya kutopaza sauti yake. Aliongeza kuwa alishangazwa na tabia ya polisi na kusema kitendo hicho cha polisi kinapaswa kulaaniwa.

"Walimleta mchochezi mbele ya msikiti wetu, na wakampa kipaza sauti. Tulisikia matusi yake ... Tulipotaka kujibu matusi yake, tulizuiwa na polisi. Ninalaani kitendo hicho," amesema katika mazungumzo na wanahabari.

Mtu mwenye misimamo mikali ambayo amekuwa akivunjia heshima Qur'ani Tukufu mara kwa mara na  anayejulikana kama Salwan Momika aliondoka eneo la tukio akiwa ndani ya gari la polisi lililokuwa na silaha, akisindikizwa na takriban magari 20 ya polisi na maafisa 100 wa polisi.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Momika kulenga Qur'ani Tukufu huko Stockholm. Alikuwa amefanya vitendo kama hivyo katika wiki chache zilizopita, kwa msaada wa mtu mwingine mwenye msimamo mkali mwenye asili ya Iraq, Salwan Najem.

Matukio hayo ya uchomaji moto wa Qur'ani Tukufu yamezusha hasira miongoni mwa mataifa ya Kiislamu na Umoja wa Ulaya ambao Usiwidi ni mwanachama. Wamelaani mashambulizi dhidi ya utakatifu wa Quran kuwa ni ya chuki dhidi ya Uislamu na uchochezi.

Habari zinazohusiana
captcha