IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Kikao cha Makka: Kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu ni kinyume cha maadili ya haki za kibinadamu

17:36 - August 16, 2023
Habari ID: 3477446
MAKKA (IQNA) - Washiriki katika Kongamano la Kimataifa la Siku mbili la Kiislamu katika mji mtakatifu wa Makka, Saudi Arabia wamelaani vikali vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu barani Ulaya na kusema ni vitendo vya kulaaniwa kwani vinakinzana na maadili ya kibinadamu yanayoshirikiwa kote ulimwenguni.

Mkutano huo uliomalizika siku ya Jumanne, ulisisitiza haja ya kuimarishwa mawasiliano, na ushirikiano wenye nguvu zaidi katika masuala ya Kiislamu miongoni mwa idara za masuala ya kidini. Mkutano huo ulifanyika chini ya kaulimbiu "mawasiliano na ushirikiano".
Taarifa ya mwisho ililaani vikali vitendo  vya mara kwa mara vya kuchoma nakala za Qur'ani Tukufu.
Washiriki walisisitiza kwamba vitendo hivyo vya kuchukiza vinachochea chuki, vinakuza mgawanyiko na ubaguzi wa rangi, na vinapingana na maadili yanayoshirikiwa kote ulimwenguni.
Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na wanazuoni wakuu wa Kiislamu wapatao 150, mamufti, viongozi wa kidini na wanafikra kutoka nchi 85.

MECCA (IQNA) - Washiriki katika Kongamano la Kimataifa la Siku mbili la Kiislamu katika mji mtakatifu wa Mecca wamelaani vikali kudharauliwa mara kwa mara kwa Qur'ani Tukufu barani Ulaya na kusema ni vitendo vya kulaaniwa ambavyo vinakinzana na maadili ya kibinadamu yanayoshirikiwa kote ulimwenguni.

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watetezi wa qurani
captcha