IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Kuvunjia heshima Qur’ani ni kitendo cha chuki dhidi ya Uislamu kwa lengo la kuchochea uhasama

21:50 - September 22, 2023
Habari ID: 3477632
NEW YORK (IQNA) – Waziri Mkuu wa Malaysia Datuk Seri Anwar Ibrahim alishutumu vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani kuwa ni vitendo vya "chuki dhidi ya Uislamu" ambavyo vinalenga kuchochea uhasama.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Anwar alisema Malaysia ina wasiwasi juu ya kuibuka kwa "aina mpya ya ubaguzi wa rangi" yenye sifa ya chuki dhidi ya wageni, na fikira potofu dhidi ya Waislamu.

Alisema kutochukua hatua mbele ya uchochezi huo wa wazi kwa dini ni kutowajibika na kunatoa ujumbe wa hatari kwa ubinadamu.

"Hii inadhihirika katika mwenendo wa kutisha wa chuki, kutovumiliana, na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya Waislamu na utakatifu wao," alisema.

Malaysia, alisema ilishangazwa na kuhalalishwa kwa vitendo hivi chini ya kisingizio cha kutetea haki za binadamu.

Waziri Mkuu wa Malaysia, amesisitiza kuhusu kuvumiliana na kuheshimiana, na pia kukuza tamaduni, ustaarabu na dini mbalimbali.

“Lazima tuunganishe imani zetu katika jambo moja ili kukuza maelewano na nia njema miongoni mwa watu wetu, na kuimarisha amani na maelewano kati ya mataifa.

"Haya ni maagizo marefu lakini ndio sababu tuko hapa. Ninaamini kweli kwamba hakuna changamoto, hata kama ni kubwa, isiyoweza kutatuliwa ikiwa tutapata dhamira ya pamoja ya jumuiya hii ya kimataifa, nchi wanachama wa taasisi hii tukufu.

"Tunachohitaji ni imani ya kuifanya dunia kuwa mahali pazuri, nia ya kufanya kazi pamoja kwenye jukwaa la maelewano na mshikamano," alisisitiza.

Aidha baada ya mkutano wa pande mbili umatano, Anwar na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan walilaani vikali uchomaji moto wa hivi karibuni wa Qur'ani Tukufu barani Ulaya .

Katika taarifa ya pamoja, viongozi wote wawili pia walielezea wasiwasi wao juu ya kuibuka kwa "aina mpya ya ubaguzi wa rangi" yenye sifa ya chuki dhidi ya wageni, na fikira potofu kuhusu Waislamu.

3485271

Habari zinazohusiana
captcha