IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Nakala ya Qur’ani iliyovunjiwa heshima Uholanzi imekarabatiwa, yakabidhiwa Balozi wa Uturuki

13:35 - September 23, 2023
Habari ID: 3477638
AMSTERDAM (IQNA) – Nakala ya Qur’ani Tukufu iliyovunjwa heshima na kuchanwa nchini Uholanzi mwezi uliopita imekarabatiwa.

Msahafu huo sasa umekabidhiwa kwa Balozi wa Uturuki nchini Uholanzi Selcuk Unal siku ya Ijumaa.

Msahafu huo ulinajisiwa na kundi la chuki dhidi ya Uislamu la PEGIDA wakati wa kitendo cha uchochezi huko The Hague mnamo Agosti 18.

Ilikabidhiwa na Salih Arslan, mkuu wa Jumuiya ya Msikiti wa Mimar Sinan, yenye uhusiano na kundi la Kituruki-Waislamu IGMG.

Unal aliiambia Anadolu kwamba kundi lake linalaani vikali mashambulizi dhidi ya Qur’ani  Tukufu na linatumai vitendo hivyo havitarudiwa tena.

“Baada ya kukarabati nakala iliyochanika ya Qu’ani Tukufu...hatutasahau kitendo hiki cha dharau na tutaihifadhi katika ubalozi wetu,” alisema.

Unal alisema wanachama wa PEGIDA wanapanga kufanya maandamano kama hayo mbele ya Ubalozi wa Uturuki mjini The Hague na balozi nyingine katika nchi za Kiislamu Jumamosi.

Wanawasiliana na mamlaka zote zinazohusika za Uholanzi ili kuzuia vitendo hivyo, alisema.

Rasmus Paludan, mwanasiasa wa Denmark wa mrengo mkali wa kulia na kiongozi wa Chama cha Stram Kurs (Msimamo Mkali), aliendelea na uchochezi kwa kuchoma Qur’ani Tukufu katika miji ya Uswidi ya Malmo, Norkopin, Jonkoping na Stockholm wakati wa likizo ya Pasaka mnamo 2022.

Paludan alichoma kitabu kitakatifu cha Waislamu mbele ya Ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm mnamo Januari 21 na katika mji mkuu wa Denmark Copenhagen mnamo Januari 27.

Edwin Wagensveld, kiongozi wa genge la  chuki dhidi ya Uislamu, Patriotic Europeans Against the Islamization of the West (PEGIDA), nchini Uholanzi, alirarua nakala ya Qur’aniTukufu katika maandamano ya mtu mmoja huko The Hague mnamo Januari 22, chini ya ulinzi wa polisi, na tena Februari  13 katika jiji la Utrecht.

Huko Stockholm, Salwan Momika alichoma moto nakala ya Qur’ani Tukufu chini ya ulinzi wa polisi mbele ya Msikiti wa Stockholm mnamo Juni 28, ambayo iliambatana na siku ya kwanza ya likizo ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Momika alikanyaga Qur'ani Tukufu na bendera ya Iraq chini ya ulinzi wa polisi mbele ya Ubalozi wa Iraq mjini Stockholm tarehe 20 Julai, na mbele ya Bunge la Uswidi Julai 31 na Julai 14.

Bahrami Marjan, ambaye ana asili ya Iran, alichoma Quran kwenye ufuo wa Angbybadet huko Stockholm Agosti 3 chini ya ulinzi wa polisi.

3485272

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watetezi wa qurani
captcha